Watu 21 wameuwawa hadi kufikia jana Alhamisi katika mapambano mapya kati ya
polisi wa kutuliza fujo na waandamanaji mjini Kiev,Ukraine wakati
mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakikutana na Rais Vikctor
Yanukovich.
Mapambano mapya yameibuka kati ya polisi wa kutuliza fujo na
waandamanaji leo hii katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, na kutibua mpango
tete wa suluhu wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
wakikutana na Rais Vikctor Yanukovich kujaribu kutafuta ufumbuzi wa
mzozo huo.
Mapambano hayo ya jana yalizuka wakati waandamanaji waliojifunukia nyuso
walipowarushia polisi wa kutuliza fujo mabomu ya petroli na mawe katika
uwanja wa Uhuru mjini Kiev ambacho ni kitovu cha mzozo wa kisiasa wa
jimbo hilo la zamani la Muungano wa Kisovieti.
Waanadamanaji hao walifanikiwa kuwarudisha nyuma polisi kwa kama mita
200 na na kuweza kuudhubiti tena uwanja huo wote ambao waanadamanaji
wanaopinga serikali walikuwa wakiukalia kwa mabavu tokea mwezi wa
Novemba mwaka jana.
Polisi ilitumia risasi za mpira kujaribu kuzima shambulio la
waandamanaji hao na imedai kwamba mashambuliaji wa kuvizia amewajeruhi
polisi 20 kwa kuwafyetulia risasi za moto kutoka kwenye jengo
linaloelekezana na uwanja huo ulipgubikwa na moshi.
Polisi ilitumia risasi za mpira kujaribu kuzima shambulio la
waandamanaji hao na imedai kwamba mashambuliaji wa kuvizia amewajeruhi
polisi 20 kwa kuwafyetulia risasi za moto kutoka kwenye jengo
linaloelekezana na uwanja huo ulipgubikwa na moshi.
Mapambano hayo yametibua suluhu waliokubaliana kati ya Rais Viktor
Yanukovych na viongozi wa upinzani masaa machache kabla kufuatia
umwagaji damu uliogharimu maisha ya takriban watu 28 katika kipindi cha
siku mbili.
Taarifa fupi iliyochapishwa kwenye wovuti wa ofisi ya rais hapo jana
usiku haikutowa maelezo suluhu hiyo inamaanisha nini au itatekelezwa
vipi na wala haikufafanuwa mazungumzo yatafanyika vipi na pia
haikodokeza iwapo yatakuwa tafauti na mikutano iliofanyika huko nyuma
kati ya rais na viongozi wa upinzani.
Mbinu za kisiasa na za kidiploamasia zimekuwa zikiendelezwa ambapo pande
zote mbili Urusi na mataifa ya magharibi zimekuwa mbioni kujenga
ushawishi wao kwa nchi hiyo. Mawaziri watatu wa mambo ya nje wa Umoja wa
Ulaya kutoka Ujerumani,Ufaransa na Poland wako Kiev leo hii kuzungumza
na pande mbili zinazohasimiana kabla ya mkutano wao wa dharura wa Umoja wa
Ulaya mjini Brussels ili kufikiria hatua za kuchukuwa dhidi
ya wale waliohusika na umwagaji damu wa hivi karibuni nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amezungumza na waziri
mwenzake wa Ujerumani Frank -Walter Steinmeier na kumtaka kutumia
mawasiliano yake ya karibu na ya kila siku na upinzani wa Ukraine
kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imeelezea ghasia hizo kuwa ni jaraibio
la mapinduzi na hata kutumia neno "mapinduzi ya kibaguzi" kwa
kuyafananisha na kusimama kwa utawala wa Manazi nchini Ujerumani hapo
mwaka 1933. Wizara hiyo imesema Urusi itatumia ushawishi wake wote
kurudisha amani na utulivu nchini humo.
Rais Barack Obama wa Marekani pia amelaani umwagaji damu uliotokea na
kuonya kwamba itaichukulia hatua nchi hiyo iwapo hali hiyo itaendelea
ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kujiuga na Umoja wa Ulaya kuiwekea
vikwazo Ukraine.
Askari wa Ukraine wakiwadhibiti wananchi
Raia wa Ukraine akirusha chupa yenye mafuta kwa askari wa kutuliza ghasia
Baadhi yawananchi wa Ukraine wakisali kutokana na machafuko nchini humo
Wananchi waliofariki wakiwa wamefunikwa kwa bendera ya nchi hiyo na pia wakiwa wamewekewa maua kwenye miili hiyo
Mapigano yakiendelea
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako