KAMATI ya Utendaji ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mvomero, imedaiwa
kumvua Uongozi Katibu wa Wilaya wa Chama hicho hicho wilayani humo,
Mrisho Ramadhani, kwa madai ya kukisaliti Chama.
Habari
toka ndani ya kikao cha siri kilichoketi Ofisi ya Wilaya zinadai, Kamati
ilimvua ukatibu Mrisho kutokana na kufanya maamuzi ya kukiunganisha
Chadema na Vyama vingine bila ridhaa ya Chama, na kumdharilisha Diwani
wake, Luka Mwakambaya.
Akizungumza
kwa masharti ya kutotajwa jina Mtoa habari wetu alisema, Mrisho
amebakiwa na Ukatibu Mwenezi wa Wilaya, amabapo suala lake limepelekwa
kwenye Mkutano Mkuu akajadiliwe na kutolewa maamuzi.
“Baada
ya Chadema kutangaza kufanya mkutano wa M4C–Opresheni ya Pamaoja Daiama
(OPD) Kata ya Mtibwa 29.1.2014, Mrisho aliacha Sera za Chadema za
kutatua kero za wakulima na wafanyakazi zilizofanywa na Mwakambaya na
kuungana na wanaokwamisha OPD.
Mkutano huo Mrisho alisema, ‘kutokana na
kero za mwekezaji wa Mtibwa kukithiri akiwacheleweshea malipo Wakulima
wa wadogo wa miwa na wafanyakazi, Chadema kimeungana na Vyama vingine
kudai haki kwa maandamano baada ya Diwani Mwakambaya kushindwa, jambo
ambalo halikuwa kweli na lilipingwa na wananchi, kwa sababu amekuwa
akilala langoni mwa lango la mwekezaji na kulazimika kuwalipa.
“Kama haitoshi, 29.1.2013,
alimdharilisha Diwani wa Kata ya Mtibwa, Mwakambaya (Chadema) katika
Mkutano hadhara, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,
aliyetaka aelewe Kero za Mwekezaji wa Mtibwa aende nazo bungeni”.alisema
mtoa habari.
Aidha baada ya Mwenyekiti wa Chadema
Wilaya ya Mvomero Saimanga Kashikashi kutafutwa bila mafanikio,
alimtafutwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Msingi Chadema, Innocent Zawadi
kutaka kujua suala hilo, naye alisema ngoja awasiliane na uongozi wa
Wilaya ya Mvomero kupata habari sahihi.
Nafasi ya Katibu wa Wilaya ya Mvomero
(Chadema) tangu uchaguzi ufanyike, imekuwa ikipyaya na kukaimishwa kwa
mara pili sasa, ambapo baada ya kikao hicho jana imekaimishwa kwa,
Rosemaary Kimune, huku wapenzi wa Chadema wakikitaka chama kutafuta mtu
makini.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako