Uchaguzi Jimbo la Kalenga waanza Kupamba Moto,Hawa 9 wamechukua Fomu CCM
Chama Cha Mapinduzi jimboni Kalenga
mkoani Iringa kimeanza rasmi mchakato wa kumpata mgombea wa ubunge wa
jimbo hilo. Uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika kufuatia kifo cha
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. William Mgimwa.
Tayari wanachama tisa wa chama hicho
wamekwishachukua fomu kuonesha nia yao ya kuingia katika kinyang'anyiro
hicho. Wanachama hao ni Hafsa Mtasiwa, Jackson Kiswaga, Godfrey Mgimwa,
Edward Mtakimwa na Thomas Mwakoka.
Wengine ni Gabriel Kalinga, Msafiri Pamagil, Peter Mtisi na Grayson Kibasa.
Chama hicho kitaendesha kura ya maoni
siku ya Jumamosi tarehe 8 Februari. Kura hiyo ni kwa ajili kupata jina
la mgombea mmoja litakalowasilishwa kwenye Tume ya Uchaguzi. Tume ya
Uchaguzi bado haijatangaza rasmi tarehe ya uchaguzi jimboni humo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako