Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limetuma barua tatu tofauti kwa Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage, moja ikiwa ni ile inayomhusu Emmanuel Okwi ambaye sasa
yuko Yanga.
Moja ya
barua ambazo Rage amepewa kopi na Fifa ni ile ambayo Shirikisho la Soka la
Uganda (Fufa), limemuomba Okwi kurejea Uganda na kuitumikia timu ya taifa
katika michuano ya kimataifa.
Pamoja na
barua hiyo, Rage amethibitisha kupokea barua hizo tatu kutoka Fifa ikiwemo ile ya
Etoile du Sahel ya Tunisia kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni la dola
300,000 wanazodaiwa na Simba kutokana na mauzo ya Okwi.
“Kweli nimepokea
barua hizo, moja ni ile ambayo Etoile ambao mwezi huu ndiyo ulikuwa mwisho kulipa
dola 300,000, sasa wameomba waongezewe muda hadi Septemba, mwaka huu ili waweze
kulipa.
“Fifa wao
wamenitumia kopi lakini barua hiyo ni kutoka kwao Etoile kwenda Fifa na
wamethibitisha kwamba ni kweli Simba inawadai,” alisema Rage.
Barua ya
tatu kati ya hizo kwa mujibu wa Rage ni ile ambayo inaonyesha namna klabu hiyo
ya Tunisia ilivyomshitaki Okwi kwa Fifa kutokana na kuonyesha kukiuka mambo
kadhaa wakati akijua mkataba wake nao unamalizika mwaka 2016.
“Katika ile
barua ya kuhusiana na suala la kulipa, Fifa wametaka tusaini na kukubali kwamba
sasa mwisho utakuwa Septemba 30 na tayari barua hiyo nimeikabidhi kwa Hans
Pope,” aliongeza Rage.
Tayari Okwi
yuko nchini na Yanga imemsajili ingawa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limeamua kusimamisha usajili wake hadi litakapopata ufafanuzi kuhusiana na
usajili wake.
Wakati Fifa
ilitoa kibali kwa Okwi kucheza SC Villa ya Uganda kwa miezi sita, lakini Yanga
ikamnunua na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, suala ambalo limezua mzozo
mkubwa huku Simba wakiendelea kusisitiza kulipwa fedha zao ambazo mwanzo
walimuuza na hawakulipwa.
Okwi
amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuichezea Yanga ambayo imemsajili, huku
akieleza amekuwa akiumia moyoni kuona wenzake wakicheza naye akiwa jukwaani
kama mtazamaji.
SOURCE: CHAMPIONI
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako