Kiungo Mtanzania nyota wa Al Markhiya inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Qatar, Mwinyi Kazimoto ameweka rekodi ya kucheza mechi 11 zote kwa dakika 90.
Kazimoto aliyetokea Simba na kujiunga na Al Markhiya, ameweka rekodi hiyo baada ya kupiga mechi hizo 11, kimahesabu, amepiga dakika 990.
Kutokana na mwendo huo, Kazimoto ameisaidia timu yake kushinda mechi tatu mfululizo na sasa iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 21.
“Mechi ya mwisho pia tumeshinda, tulicheza dhidi ya timu ambayo ni ngumu na inapewa hata nafasi ya kutwaa ubingwa.
“Kadiri ligi inavyosonga ukingoni, mambo yanazidi kuwa magumu kwa kuwa ushindani unaongezeka,” alisema.
Kazimoto ameaminika katika kikosi hicho licha ya kuwa na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani, ndiye amepewa dimba la juu, yaani namba nane.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako