Msanii
kutoka Sudan, K Denk ambaye amejijengea jina Kubwa Afrika Mashariki
akiwa mshiriki wa mashindano ya Tusker Project Fame, amewashtusha wengi
kwa hatua yake ya kuamua kuingia vitani katika mapambano yanayoendelea
sasa huko Sudan Kusini akiwa kama muasi.
Msanii huyu ambaye jina lake halisi
ni Kuonck Deng ameweka picha zake katika ukurasa wake wa facebook akiwa
ameshikilia silaha kali (Bunduki aina ya AK47) tayari kwa mapambano
katika kile alichokiita kama kupigania uhuru wake.
Kufuatia kuweka picha hii mtandaoni, K
Denk amepata maoni mbalimbali yanayokosoa hatua yake hii hususan kutoka
kwa mastaa/washiriki wenzake kutoka Tusker Project Fame akiwepo
Ngangalito na Juvenalis kutokana na ukweli kuwa vita sio suluhisho la
matatizo yaliyopo huko Sudan kwa sasa.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako