A

A

Minziro, Mogela waula TFF



Shirikisho la Soka (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa kuboresha timu ya taifa (Taifa Stars).

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya shirikisho hilo zilizopo Karume jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema makocha hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalum ya mikoa, wanatakiwa kuripoti katika ofisi za TFF Jumamosi asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo zaidi.

Waliokuwa makocha wa Yanga, Fred Minziro na Rhino Rangers, Sebastian Nkoma pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Soka cha Rollingstone cha jijini Arusha, Ally Mtumwa na kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Ali Bushiri, ni miongoni mwa wateule wa jopo hilo la wataalm wa soka.

Wambura aliwataja walioteuliwa kuwa ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Bushiri (Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani (Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).


Elly Mzozo (Dar es Salaam), Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es Salaam).

Kenny Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera (Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).

Wengine ni Peter Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan (Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es Salaam).

Uteuzi huo umefanywa ili kutekeleza mapendekezo ya jopo la wataalam wa soka walioketi visiwani Zanzibar Novemba mwaka jana kutafuta njia za kusaka wachezaji bora ili kuiimarisha Taifa Stars.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako