Yelewiii!
Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini
jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya
mapenzi na changudoa ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.
Dereva
huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa
Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo
kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.
OFM
ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya
Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti’ namba upande wa mbele) mali ya
kampuni hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na
kupaki gari kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.
Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama
kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa
doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru
dereva ashuke.
Hata
hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha
vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya
gari.
Askari
waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona
mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika
mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa
naye.
Akizungumza
kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa
kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si
kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva
huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na
changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa
kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo
walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.
Alipohojiwa
changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua
kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya
kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika
hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake
(Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili.
gpl
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako