"Dunia ya sasa imegubikwa na utandawazi ambao kuanzia shule za msingi wanatumia Laptop,sasa ningependa Ipad, ilikupunguza gharama zinazotumika na Bunge kuchapisha nyaraka mbali mbali".
"Lazima wanafunzi wa shule na vyuo wajifunze kutoka kwetu,sasa wanatushangaa tukiendelea kutumia utaratibu huu wa kugawiana makaratasi yenye nyaraka litakuwa jambo la kusikitisha,nina imani tukipatiwa vifaa hivyo watendaji watakuwa wanatutumia ujumbe wa taarifa tunazopaswa kujadili au kazi tulizopangiwa kufanya," alisema.
Hata hivyo,mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo,mh.Kificho alipinga wazo hilo kwa maelezo kuwa utaratibu huo ni wa gharama zaidi.
CHANZO:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako