Star wa filamu Swahiliwood, Rose Ndauka
amemuweka hadharani mtoto wake aliyejifungua hivi karibuni na kumpa jina
la Naveen yeye na
baba mtoto wake Malick Bandawe(Chiwaman). Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Rose aliweka picha ta mwanae jioni hii na kuandika "nachukua nafasi hii kuwashukuru wote mlioweza kuwa na mimi na mpaka sasa tumepata mtoto wetu anayeitwa naveen na leo ikiwa tunasogelea arubaini yake tarehe 9/02/2014

basi nawaomba dua zenu na hii ndio zawadi niliopata kwa mungu nashkuru sana kwa zawadi hii shukran mama yangu mzazi na
malick kwa zawadi hii... nawapenda sana
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako