A

A

Huko Instagram Mwanamziki T.I amtolea Uvivu Mke wake kwa Picha hizi


Clifford Joseph Harris Jr. aka T.I, rapper wa Atlanta Marekani, ameshindwa kuvumilia baada ya kuona mke wake ‘Tiny’ amevuka mipaka kwa kupost kwenye Instagram mfululizo wa picha zinazoonesha makalio yake.

Ingawa rapper huyo toka Atlanta alikuwa na uwezo wa kumpigia simu ama kumtumia message mkewe huyo kumuonesha alichokuwa hapendi kwenye picha hizo, jamaa aliona dawa inatakiwa iwekwe pale pale kwenye kidonda! Hivyo akaandika pale pale palipomuudhi!!

“You have so much more going for u other than your a$$. Although it is so magnificent, I think u should spend just as much time showcasing those other things as u do ya #booty…awesome pic thou. Lov.” Ameandika T.I kwenye post hiyo.

Mkewe Tiny nae akamjibu kwa kung’ata na kupuliza, kwa kuwa inasemekana kuwa ameshachoshwa na ugomvi uliopo katika ndoa yake.

Alimjibu kwa kejeli T.I kuwa yeye hakuwa na nia ya kuonesha makalio yake bali alikuwa anataka kuonesha kiuno chake, na kwamba kumbe mmewe alikuwa anaangalia makalio tu.

“I wasn’t showing off my ass in this pic it was about my waist… u just looking at the ass bae! U know I wasn’t saying getting my sh*t together about my ass now don’t U? But glad u like it bae.”

Majibishano hayo kati ya wanandoa na mastaa wa kipindi cha TV cha Family Hustle kinachowaunganisha wao na watoto wao saba, yalisababisha mashabiki wao kushangaa na wengine walitoa ushauri kuwa T.I angetakiwa kutumia simu.

Tangu mwezi uliopita kumekuwa na ripoti kuwa wawili hao wako katika mgogoro mkubwa kiasi cha kusemekana kuwa wanataka kupeana talaka.

Tetesi hizo zilichochewa na picha za Tiny alizopost zikionesha mkono wake wa kushoto ukiwa bila pete ya ndoa. Iliripotiwa pia kuwa mwanamke huyo anaewaelewa watoto saba wa T.I na wake kwa ujumla wao, amekuwa akiparty sana akiwa na rafiki zake, tofauti na zamani

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako