Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda,
Emmanuel Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
Katibu
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ameiambia BIN
ZUBEIRY muda huu kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni
halali kuchezea Yanga SC.
“Suala
la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye
kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema
Mwesigwa.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF iliyokutana Januari 22, mwaka
huu kupitia masuala mbalimbali, ilisema imesimamisha usajili huo baada
ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali
maalumu kutoka FIFA.
Okwi
ambaye aliingia kwenye mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya
Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu
(provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati
suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo
la kimataifa.
Kulikuwa
kuna kesi tatu FIFA kuhusiana na suala la mchezaji huyo, Okwi
ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel
imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du
Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola
za Marekani 300,000.
Hivyo,
TFF iliiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza
Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika
shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake na majibu
yamewasili TFF Mganda huyo akihalalishwa kuendelea na kazi Yanga

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako