A

A

Binti ashikwa na “wazimu” kwa kunyimwa ngono?

Huko mjini Glendale (hapa Arizona) katika mwanamke mmoja ameruhusiwa kutoka jela baada ya kuzuiliwa kwa kosa la kuvua nguo zote na kubakia utupu kwa hasira zilizotokana na kukataliwa tendo la ndoa na rafikiye wa kiume.

Maafisa wamesema bibi huyo mwenye umri wa miaka 24 alikamatwa Jumatatu kwa hofu kuwa huenda atawadhuru mtoto na rafiki yake wa kiume, kuhatarisha usalama, shambulio lenye nia ya kudhuru, uharibifu na kuwa katika mwenendo usiofaa.

Aliachiliwa siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashitaka kortini na kung'amua kosa lake.

Awali, polisi walipofika katika makazi ya msichana huyo, walimkuta akiwa uchi, amelewa huku mikono yake ikiwa na damu iliyotokana na kujiumiza wakati akipiga ngumi ukuta na kwenye vioo vya picha za ukutani.

Ilielezwa kuwa, rafiki yake wa kiume alipokataa kufanya ngono, binti huyo alimnyanyua mtoto wao (miezi 4), na kuanza kukimbia kama mwehu ndani ya nyumba huku akisema kwa sauti kubwa na kupiga kelele. Mtoto huyo aligongwa kichwa kwenye meza ya vipodozi.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako