A

A

Wafuasi wa mirengo inayotofautiana CHADEMA waendelea kulabuana


 
Wafuasi wa CHADEMA wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam punde tu Mahakama hiyo ilipoahirisha hadi leo, kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA.

Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wanachama wa makundi yote waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na
kushangilia lakini walipofika eneo la Mahakama ya Rufani ghafla walianza kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na vurugu hizo.

Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi katika viwanja vya Mahakama tayari kusikiliza uamuzi huo. Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi walikuwa wametanda. Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa pamoja na gari la maji ya kuwasha.

Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia ndani ya u`kumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha majina yao huku wakitambuliwa na viongozi wao waliokuwapo

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako