Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.
1.
Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta
usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa
wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango
cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.
2.
Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika
kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni
sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo
makazini.
3.Gharama
za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda
kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya
kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha
gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha
gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia
gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/=
na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea
kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.
Kampuni
ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la
matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari
binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea
usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.
Hapa
City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi,
kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji.
Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.
Njia tunazotoa Huduma kwa sasa.
TEGETA - POSTA - TEGETA (kupitia MWENGE)
GONGO LA MBOTO - POSTA - GONGO LA MBOTO
MBEZI KIMARA - POSTA - MBEZI KIMARA
MBEZI AFRICANA - POSTA - MBEZI AFRICANA (kupitia Mbezi chini)
MBAGALA - POSTA - MBAGALA
TABATA SEGEREA - POSTA - TABATA SEGEREA
MWENGE - POSTA - MWENGE (kupitia Sinza)
Njia zinazotazamiwa baadae
MBAGALA KIJICHI - POSTA - MBAGALA KIJICHI
KUNDUCHI - POSTA - KUNDUCHI
Njia nyingine zitaongezwa kwa kuzingatia upatikanaji wa wateja na mahitaji
Gharama / Bei
Bei
zetu zinatazamiwa kuwa ni bei nafuu kwa kua kila mtu analipa kwa kile
anachotumia peke yake. Tiketi zetu zinapatikana kwa Tsh. 5500/= kwenda
na kurudi kwa siku kwa njia fupi, na Tsh. 11000/= kwenda na kurudi kwa
njia ndefu. Pia unaweza kujipatia tiketi za kwenda peke yake au kurudi
kwa Tsh. 3300/=. Na kwa wale ambao wangependa kujipatia tiketi za wiki
nzima (yaani siku 5) au mwezi mzima (yaani siku 20) tiketi hizi zina
unafuu wa aslimia 10%. Tiketi zinapatikana kwa mawakala wetu au kwa
kutumia simu yako ya mkononi. Au piga simu +255 715 400 666.
Tiketi
hizi zinamaanisha kuwa tutakuchukua kutoka karibu na nyumbani kwako
kukuleta mjini asubuhi na kukurudisha jioni, na kama unakaa mbali na
barabara kuu, tutakupatia sehemu salama ya kuegesha gari lako bila
wasiwasi.
Muda.
Tunahakikisha
unakua mjini kila siku asubuhi kabla ya mida ya saa 1:00 asubuhi, hivyo
basi tutakua tukiondoka maeneo tofauti jijini kwa muda tofauti
kulingana na umbali na miundo mbinu ya eneo husika, (kuanzia mida ya
11:00 asubuhi na 12:30 asubuhi) vilevile tunatoa safari ya 7:30 asubuhi
kwa wale wanaopenda kuchelewa kuingia mjini.
Kwa jioni magari yanaondoka kuanzia saa 11:00 jioni na 11:30, vile vile kuna magari ya 1:30 usiku kwa wale wanaochelewa au wafanyakazi wa mabenki. (Unaweza kuwasiliana na mtoa huduma wetu ili kuangalia upatikanaji wa safari kuendana na mahitaji yako. +255 715 400 666)
Tiketi
Tunatoa
aina mpya ya tiketi zinazowekwa QR codes kwa ajili ya usalama, na
unaweza kuzipata kwa mawakala wetu, au kwa kununua mwenyewe kupitia
namba yetu ya simu +255 687 644452 na
utatumiwa tiketi yako kwenye simu yako ya mkononi, au barua pepe au
hata kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukamilisha malipo, na
utatakiwa kuonyesha tu QR codes uliyotumiwa kwa ajili ya uthibitisho. Ni
rahisi kiasi hicho.
Kumbuka
hautaweza kulipia ukiwa ndani ya gari, na kuna idadi maalumu ya wateja
watakaohudumiwa kwa siku, hivyo ni muhimu kama utaweka siti yako mapema
kuepuka usumbufu.
Kwa
maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi zetu zilizoko kwenye jengo la
NSSF Hifadhi house gorofa ya Saba, karibu na mnara wa askari, au ukapiga
simu namba. +255 222 114 308 Mobile: +255 712 823 505 au barua pepe: cityridezsales@gmail.com, au tembelea kuras wetu wa facebook:www.facebook.com/cityridez
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako