Naibu Waziri Mh:mwigulu Nchemba ,Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara hii leo ameshiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo aliyefariki mapema wiki hii Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya Kuugua kwa Muda Mrefu.Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi na Upinzani amemzungumzia Marehemu Kuwa "Ameondoka kipindi ambacho Wanachalinze bado wanamuhitaji,Chama Cha Mapinduzi bado kilikuwa Kinamuhitaji kutokana na Mchango wake Mkubwa kwenye Ujenzi wa Chama pale Chalinze,Pia Uwakilishi wake kwa Wananchi ulikuwa ni Wakuigwa Mfano kutokana na Ukubwa wa Jimbo lenyewe la Chalinze,Hivyo Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi."
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Mh:Koka Mbunge wa Kibaha Mjini(Kushoto) kwenye shughuli ya Mazishi ya Aliyekuwa Mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo.
Mh:MWigulu Nchemba akizungumza na
Mh:Mwigulu Nchemba wakisalimiana na Mh:Freeman Mbowe hii leo Msibani kwa Marehemu Said Bwanamdogo aliyekuwa Mbunge wa Chalinze.
Picha Zote na HABARI KWANZA BLOG
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako