Rais
wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine akiwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na Kupokea na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kuhudhuria kilele
cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na mgeni
wake Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine kwenye
chumba cha watu mashuhuri { VIP } hapo uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya
Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine akisalimiana na baadhi ya wana
jumuiya ya Wakfi ya Wangazija hapa Zanzibar waliofika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Zanzibar Kumpokea.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Rais wa Jamuhuri ya
Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine amewasili Zanzibar
leo jioni kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za kutimia
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Kilele cha maadhimisho
hayo kitafanyika katika uwanja wa amani Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa
na maelfu ya wananchi, viongozi wa kiserikali, siasa pamoja na wageni
waalika kutoka baadhi ya nchi za kiafrika na zile rafiki.
Kwenye uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Mheshimiwa Dr. Ikililou alipokewa na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif pia
aliambatana na Baadhi ya Mawaziri, makamanda wa Vikosi vya aUlinzi na
usalama Nchini pamoja na Wanajumiya ya Wakfi ya Wangazia hapa Zanzibar
wakiongozwa Rais wao Profesa Saleh Idriss Ahmed.
Mara baada ya kuwasi
Rais huyo wa Jamuhuri ya Comoro na mwenyeji wake Balozi Seif
waliangaliwa kikundi cha ngoma za asili kilichotayarishwa rasmi kwa
ajili yake.
Jamuhuri ya Comoro
imekuwa na uhusian wa muda mrefu na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa
kutokana na wananchi wake kuingiliana kidamu jambo ambalo linafanya
watu wa pande hizo mbili wawe kama ndugu wa familia moja.
Mheshimiwa Dr.
Ikililou Dhoinine anatarajiwa kurejea nyumbani Comoro kesho jioni mara
baada ya sherehe za maadhimisho hayo ya miaka 50 ya mapinduzi matukufu
ya Zanzibar.