Hamisa Hassani Mobeto amezaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza
na kabila lake ni Mnyamwezi. Mwanzo wake katika tasnia ya u-miss na
modelling ilianza baada ya hamisa kuibuka mshindi wa shindano la Miss
XXL BACK TO SCHOOL BASH Mwaka 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL
kutoka Clouds Fm. Mwaka 2011 Hamisa alishiriki mashindano ya Miss Dar
Indian Ocean na alifanikiwa kushika nafasi ya pili , pia mwaka huohuo
alikua mshindi wa pili wa miss kinondoni na kufanikiwa kuingia kwenye
Nusu fainali ya miss Tanzania.
Mwaka 2012 hamisa alishiriki kwenye mashindano ya
Miss Univeristy Afrika na kuingia hatua ya 10 bora.
Kutokea Hapo hamisa amekuwa gumzo kwenye tasnia ya uanamitindo na
filamu pia. Pia amisa ni video vixen na wengi mnaweza kumuona kwenye
video ya Quick Rocka ya My Baby.
Mwaka 2014 umeanza vizuri kwa Hamisa baada ya kuweza kutokea kwenye
cover page la Pulse Magazine la Nchini Kenya. Akiwa Ndio kwanza ana
miaka 21 Hamisa ni mtu wa kuangaliwa sana huu mwaka sababu anategemewa
kufanya mambo makubwa zaidi.