A

A

Mjadala: Kitabu cha "Cheche: Reminiscences of a Radical Magazine"

Ukarasa wetu wa ‘Kitabu Nilichosoma’ unakuletea mjadala wa kitabu cha ‘’Cheche: Reminiscences of a Radical Magazine’’. 


Kitabu kinazidurusu harakati na fikra za kina Issa Shivji, Karim Hirji , Yoweri Museveni, Zakia Meghi , Henry Mapolu nk chini ya chama chao cha kiharakati cha ‘’University Students Revolutionary Front-USARF’’ enzi za ujana wao Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  • Je fikra zao zina nafasi yeyote kwa vijana wa sasa?
  • Kulikuwa na mafanikio na mapungufu gani kwenye fikra na harakati zao?

Mjadala husika utawaleta pamoja vijana wa

sasa na wale wa miaka ya 60, 70 na 80 kuzichambua fikra na harakati za 
wana-USARF na kutathmini uhalisia wake kwa kizazi cha leo.

MAHALI: Ukumbi wa TGNP, Mabibo, Dar es salaam ( Karibu na Chuo cha Usafirishaji-NIT)

SIKU: Jumamosi, Tarehe 11/1/2014

MUDA: Saa 4.00 Asubuhi- Saa 7.00 Mchana

MGENI RASMI: Profesa Karim F. Hirji Mhariri/ Mmoja wa watunzi wa Kitabu

WAGENI WAALIKWA: Wanajamii wote


MUHIMU: Kwa wanaopenda kuhudhuria, ni muhimu kuthibitisha ushiriki kwa mawasiliano yafuatayo:
Ado Shaibu ( 0653619906) au Seif Abalhassan (0717577517).

KARIBUNI SANA