Ofisa
mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki
wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni
hiyo China Bwana Cheng Wang Wu kushoto akiwasili kwenye uwanja wa ndege
wa Mwalimu J.K.Nyerere huku akiwa ameongozana na Meneja Mkuu wa
kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wakilakiwa na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande, kampuni hiyo
imeanzishwa nchini ikiwa na lengo la kuwakomboa na kuwasaidia wafanya
biashara wadogo na wa kati nchini Tanzania ili kutafuta masoko na kuwapa
taarifa sahihi za masoko na biashara nchini China ambapo wanatarajia
kuendesha semina kwa wafanya biashara katika mikoa ya Dar es salaam,
Arusha, Mwanza na Mbeya.
Meneja
Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akizungumza na
waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara
baada ya kwasili akitokea nchini China na ujumbe wa wafanya biashara
wenzake, kushoto ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu na kulia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande wa pili kutoka kulia ,Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wa tatu kutoka kulia na Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu wa tatu kutoka kushoto wakiwa na wafanya biashara wenzao.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.