Na
Beda Msimbe — WAFUASI wa CHADEMA, leo waligeuza eneo la Mahakama Kuu ni
la kuoneshana ubabe baada ya kukunjana na kupigana kabla ya kesi
ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kuanza kusikilizwa
Mahakamani hapo.
Kabla hata hawajakunjana wafuasi hao walitumia nafasi hiyo kumzomea mbunge huyo wakidai kesi aliyofungua dhidi ya chama hicho inawacheleweshea muda.
Vurugu hizo zilianza saa 3 asubuhi baada ya Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi saa 4, ndipo wafuasi hao walipomfuata Zitto kumfanyia fujo jambo lililosababisha askari wamchukue na kumhifadhi katika chumba maalumu kwa usalama wake.
Wakili wa CHADEMA, Tundu Lissu aliwaita wanachama hao na kuwasihi watulie wasikilize walichoitiwa mahakamani hapo ili wasizuiwe kuingia mahakamani, hata hivyo kwa ujasiri saa 5.50 wafuasi hao walianza tena vurugu na kutaka kumpiga askari kanzu wakidai anawarekodi.
Balaa likawa kubwa zaidi pale mmoja wa wana CHADEMA alipomtetea askari huyo, kwani kibao kikamgeukia na kutandikwa hadi kumchaniwa shati.
Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Wilibrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako