A

A

Baada ya Kubwagwa Mahakamani,Mwenye Chama anena "Zitto hatakiwi CHADEMA"


"Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake
au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.
Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute
vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.
Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida...
“Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.
”Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua
mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho." Mwisho wa kunukuu.

My take: Je CHADEMA kama chama ni mali binafsi ya Mzee Mtei ama Wananchama? Kama ni mali ya wanachama, huo ujasiri wa Mzee Mtei kudai kwamba mwanachama fulani hatakiwi ndani ya chama anatoka wapi? Tujadili.​

source: Zitto aibuka kidedea mahakamani - Kitaifa - mwananchi.co.tz


Update: Kauli nyingine iliyopatwa kutolewa na Mzee Mtei dhidi ya Mhe. Said Arif alipojivua Umakamu mwenyekiti kwa kutuhumiwa kumsaidia Mhe. Pinda kupita bila kupingwa uchaguzi wa 2010 na Kupinga Mzee Mtei kumchagulia watu wa kufanya nao kazi. "Aache Kulalamikia, kwasababu wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, alipaswa kujichunguza kwanza."

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako