A

A

VIDEO; ROSE MUHANDO AJA KWA STYL NYINGINE, AACHIA VIDEO MPYA "WOLOLO" CHINI YA SONY MUSIC AFRICA



Muimbaji wa muziki wa injili nchini Rose Muhando hatimaye amevunja ukimya kwa kuachia video chini ya label ya kimataifa inayomsimamia kwa sasa Sony Music Africa.
Hivi karibuni Bongo5 ilizungumza na Mkuu Wa Vipaji na Biashara Mpya wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha, ambaye aliahidi kuwa kazi mpya za Rose zitaanza kutoka mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni tarkribani miaka miwili toka muimbaji huyo asaini ‘record deal’ na label hiyo ya kimataifa.
Video ya Rose Muhando ‘Wololo’ pia imekuwa certified na mtandao wa video za muziki wa Marekani VEVO. Video hii imepandishwa youtube December 13 kupitia channel ya RoseMuhandoVEVO.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako