KWA TAARIFA YAKO hii leo ina mhusu mwimbaji nyota ambaye ana
album mbili tangu aanze huduma ya uimbaji na album zote mbili zimekuwa
zikipendwa na watu wengi, huyu si mwingine bali ni Martha Mwaipaja au
mwite mama mchungaji John Said. Mwimbaji huyu ana mengi na mazito
aliyopitia katika utoto wake mpaka kufikia hapo alipo. Martha amekuwa
akiimba nyimbo za kutia moyo sana kuliko za shangwe kama baadhi ya
waimbaji wengine wanavyofanya, nyimbo zake nyingi ni za kutia moyo hasa
kwa watu wanaopitia magumu mbalimbali kama ukisikiliza wimbo wake wa
"Tusikate tamaa" katika album yake ya "Kwa msaada wa Mungu tunashinda"
vivyo hivyo ukisikiliza album yake ya pili kama wimbo uliobeba album
"Ombi langu kwa Mungu".
KWA TAARIFA YAKO sasa kama ulikuwa hujui ni kwamba kutokana na
maisha aliyoishi Martha ya kunyanyasika yeye, mama yake na wadogo zake
kukosa hela ya kula,kukosa pesa ya kwenda shule hii ni baada ya baba
yake kufariki dunia pia mama yake mzazi kukataa kurithiwa na mwanaume
mwingine (mila za zamani za Kinyakyusa au labda wengine bado
wanaziendeleza) kitendo hicho cha kukataa kiliwafanya wapate matatizo
zaidi likiwemo nililolitaja mwanzoni lakukosa pesa ya kula kuna wakati
walifanyiwa vituko vingi ili mradi tu wahame kwenye nyumba waliyokuwa
wakikaa ilifikia kuna wakati walilala hata nje. Kwahiyo kutokana na
shida zote hizi alizopitia hadi kufikia hapa alipo amekuwa na mzigo
mzito kwa watoto waliofiwa na wazazi wao au wanaoishi katika mazingira
magumu na watu wengine wanaopitia shida alizopitia.
Akiwa katika kanisa la Ufufuo na Uzima ambalo ndio kanisa lake alikotoka
baada ya kuolewa na mchungaji John Said aliweza kuandaa album ya kwanza
akitanguliza wimbo wa "Tusikate tamaa" wimbo ambao ulianza kupigwa
kupitia kipindi cha Ipo njia na Njoo tusemezane vyote vya WAPO Radio FM
mtangazaji aliyeutambulisha wimbo huo akiwa Silas Mbise ambaye naye
alivutiwa sana na wimbo huo kiasi cha kuupiga kila alipoingia studio na
ndani ya mwezi mmoja tangu aanze kuupiga mfululizo ukashika masikio na
myoyoni mwa watu kisha Martha akamaliza album yake ambayo imefanyika
baraka sana kwa watu wengi kutokana na jumbe zilizojaa katika nyimbo
hizo.
KWA TAARIFA YAKO baada ya kuolewa kwake Martha Mwaipaja na
mchungaji kuna watu walidhani kwamba itakuwa ndio mwisho wayeye kuimba
ama kutoonekana katika majukwaa ya uimbaji la hasha Martha amekuwa
akipewa sapoti ya kutosha na mumewe katika uimbaji kama ilivyoshuhudiwa
katika uzinduzi wa album yake ya pili katika viwanja vya Mwalimu JK
Nyerere ambako mumewe alikuwa sambamba lakini kama haitoshi unaweza
kumuona mumewe Martha ndani ya video yake ya Ombi langu kwa Mungu.
Ambapo kupitia maswali aliyoulizwa na wasomaji wa GK kuhusu anaonaje
maisha yake kama mke wa mchungaji na zamani kabla hajaolewa, Martha
amesema anaona utulivu ambao ameupata na anauona katika ufahamu wake
sasa hivi tofauti na zamani lakini pia ndoa yake anaona kama daraja la
kumfikisha mbali zaidi kihuduma. KWA TAARIFA YAKO ombi lake kuu
Martha ni kuona Mungu anawakumbuka watoto wanaopata shida na matatizo
mbalimbali na kwasasa lengo lake ni kufungua shule itakayowasomesha
watoto hao na pia kufanya misaada mbalimbali
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako