A

A

UZINDUZI RASMI WA MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2013 , KINGOLWIRA MOROGORO WAFANA


 Bwana Ali Masoud au Maarufu kwa Jina la' Masoud Kipanya' na ambaye Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus, akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013 Kingolwira Morogoro , pia kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka kufanya uzinduzi huo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza pamoja na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni mbalimbali waliotoka sehemu mbalimbali Tanzania na kutoa tamko rasmi la  kuzindua  shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013
Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Matha Mwasu aliyeshika nafasi ya kwanza , Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013, pia akieleza Jinsi alivyoweza kushinda na kupata mafanikio makubwa kutoka katika shindano la kizalendo la Maisha Plus.
 Mshindi wa Shindano la Maisha Plus Bernick Kimiro akizungumza na wageni wa alikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimesha anza kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Mtaalam wa Mambo ya Mbogamboga na Mshauri katika maswala ya kilimo kutoka OXFAM Bwana Zephaniah akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula 2013 , na kueleza faida za kilimo na kuwekeza kwa wakulima wodogo wadogo.
Dr. Emmanuel Tumusiime kutoka OXFAM akifanya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya 'Feed the Future Initiative in Tanzania' ambapo katika ripoti hiyo kuna mambo ya msingi ya kulinda chakula kisije kikaja kuisha na Taifa likaja kukosa kabisa siku za mbeleni.
 kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako