A

A

Usalama wa raia shakani zaidi: Polisi wawili mbaroni kwa kumteka nyara mzee


MAAFISA wawili wa polisi wamekamatwa mjini Eldoret nchini Kenya kwa  kosa la kumteka nyara mzee mmoja  mjini humo na kudai Sh200,000 kutoka kwa familia yake ndio waweze kumwachilia huru.

Afisa mkuu wa polisi Eldoret Magharibi, Bw Ndungu Wa Ikonya alithibitisha kuwa maafisa hao wameshikiliwa.

Alisema mwathiriwa alikuwa amempigia mkewe simu akitaka apelekewe pesa hizo mahali alipokuwa amefichwa.

Bw Wa Ikonya alisema kuwa mke wa mzee huyo alipiga ripoti kwa polisi  ambao waliandamana naye hadi alikokuwa amezuiliwa na kuwakamata washukiwa: “Wakati tulipata habari kuhusu tukio hilo tulielekea hadi nyumba alikokuwa amezuiliwa mzee na kuwatia mbaroni wahusika,” alieleza.

Aliongeza kuwa walipata KSh28,000 pesa bandia pamoja na dola za Kimarekani 5,200 katika chumba hicho ambapo mwathiriwa alikuwa amefungiwa. Maafisa hao wanapangiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika. --- SwahiliHub

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako