A

A

Simbachawene: Kondakta, mjasiriamali hadi kuwa Naibu Waziri


...Mojawapo ya simulizi ya kusisimua katika maisha ya Simbachawene ni ukweli kwamba aliwahi kuwa kondakta wa mabasi na bado wapo watu mkoani Dodoma wanaomfahamu kama “George Kondakta.”

“Sijawahi kujutia hata siku moja maisha ambayo nimepitia kwani yote ndiyo yamenifikisha hapa nilipo. Niliwahi kufanya kazi kama kondakta kwenye kampuni ya shemeji yangu ambaye sasa ni marehemu aliyejulikana kwa jina la Joseph Chove.

“Mabasi yale yalikuwa yakifahamika kwa jina la Urafiki Bus Service. Nakumbuka hakukuwa na masuala ya tigo au m-pesa wakati ule na watu wengi walikuwa wakitumia sana mabasi kusafirisha pesa na mizigo yao.

“Watu walikuwa wakija kwenye ofisi zetu na kuuliza kama kondakta George anasafiri au hasafiri. Kama nasafiri, mizigo mingi
sana ilikuwa ikipokewa na siku ambayo sipo, mizigo ilikuwa ikipungua. Watu walijenga kuniamini kwa sababu  ua uaminifu na nidhamu niliyoijenga kwenye kampuni hiyo.

“Kumbukumbu kubwa ambayo nimeiacha kwenye kazi yangu ya ukondakta ni kwamba mimi ndiye mwanzilishi wa njia ya Dodoma-Arusha kupitia Chalinze. Zamani watu walikuwa wakipanda mabasi ya kwenda Arusha kupitia Kondoa na ilichukua zaidi ya siku nzima.

“Nikitumia basi aina ya Leyland DAF, lenye namba zinazoanzia na TZC, nilipita njia ya Chalinze na tukafika Arusha siku hiyo hiyo saa moja usiku. Njia hiyo ilikuwa haijawahi kutumika kabla na mabasi yanayotokea Dodoma lakini baada ya ubunifu huo, leo ndiyo njia inayotumika. Nilitumia njia hiyo wakati wa sherehe za sikukuu ya Krismasi mwishoni mwa miaka ya 1990,” anasema kwa kujivunia.

Zaidi ya kazi yake hiyo ya ukondakta, Simbachawene alijiingiza kwenye biashara ya kununua na kuuza nguo. Akinunua nguo kutoka visiwani Zanzibar mwishoni mwa miaka ya 1990, na kuja kuziuza Dar es Salaam na nyumbani kwao Mpwapwa.

Mwaka 1999, mbunge huyo akahamia katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam na akapanga nyumba katika eneo hilo. Hapo ndipo alipoanza biashara nyingine, akishirikiana na rafiki yake Dk. Silveri Mwakimata; ya kufungua duka la dawa na baadaye zahanati iliyojulikana kwa jina la Vingunguti Muzdalifa Charitable Dispensary kilichopo eneo la Vingunguti reline.

Pamoja na kufungua zahanati hiyo na kuwa na biashara yake ya nguo, roho ya ujasiriamali aliyonayo ilimwonyesha fursa nyingine mahususi iliyopo Vingunguti; biashara ya mbuzi. Alifanya pia biashara ya mbuzi.

Makala nzima ipo kwenye gazeti la RAIA MWEMA

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako