A

A

Marekani yaichimba mkwara Uganda, yaitaka serikali isiupitishe muswada wa ushoga

Marekani imeitaka serikali ya Uganda kuacha kuupitisha muswada wa ushoga ambao jana ulipitishwa na bunge la nchi hiyo.
Msemaji wa serikali ya Marekani ameliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa Marekani inaheshimu uhuru wa nchi hiyo lakini inapinga sheria yoyote inayozuia uhuru wa mtu kufurahia haki zake za binadamu.
Maelezo yake yalidai kuwa taasisi nyingi za serikali ya Uganda zimezungumza kupinga uharamishaji wa ushoga.
Jana wabunge wa Uganda waliupitisha muswada wa kuzuia ushoga nchini humo. Muswada huo unapendekeza kifungo cha maisha kwa mashoga au kifo kwa wale wanaorudia makosa hayo.
Kama muswada huo ukipitishwa na rais Yoweri Museveni, mtu yeyote atakayeshindwa kumripoti mtu anayejulikana kuwa shoga naye anaweza kushtakiwa.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako