A

A

Rais Kikwete ametua Dk Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuala Lumpur, Malaysia.

Uteuzi huu umefanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi iliyoachwa na Balozi Abdul Cisco Mtiro, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Mteule Dkt. Aziz Mlima ni Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin Willi Mkapa.

----- Mwisho----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM

11 Desemba, 2013

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako