Rais Dkt Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameyaalika na kuyakaribisha makundi mbali mbali katika jamii
kupendekeza majina ya watu ambao Rais atayafikiria katika uteuzi wa
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Rais Kikwete ametoa mwaliko huo kulingana na mamlaka anayopewa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83) na aliutangaza rasmi mwaliko huo katika Gazeti la SerikaliNa. 443 la Ijumaa iliyopita, Desemba 13, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Desemba 20, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, mwaliko huo ambao pia utatangazwa katika magazeti ya kawaida, makundi yaliyokaribishwa kutoa mapendekezo yametakiwa kuwasilisha kwa Rais orodha ya watu wasiopungua wanne na wasiozidi tisa kwa kila kundi.
Makundi hayo ambayo yametajwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni Taasisi zisizokuwa za Kiserikali, Taasisi za kidini, Vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Taasisi za elimu ya juu, Makundi ya watu wenye ulemavu, Vyama vya wafanyakazi, Vyama vinavyowakilisha wafugaji, Vyama vinavyowakilisha wavuvi, Vyama vya wakulima na Makundi mengine yenye malengo yanayofanana.
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa katika kuwasilisha mapendekezo ya majina yao, makundi yaliyoalikwa yanalazimika kuonyesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu anayependekezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Katika mwaliko wake, Rais Kikwete ameelekeza kuwa orodha ya majina ya wanaopendekezwa, iwasilishwe kwa maandishi ama kwa kupelekwa na mtu kwa mkono ama kwa kutumia huduma ya Posta.
Orodha hizo ziwasilishwe kupitia anuani zifuatazo:
1.
Katibu Mkuu Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
Dar Es Salaam
ama
2.
Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
Zanzibar
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa tarahe ya mwisho ya kupokea orodha ya majina yanayopendekezwa ni Januari 2, 2014.

***************************************************************************
Special Parliament Session for Constitutional Review
Dear All,
The President of the United Republic of Tanzania, Honorable Jakaya Mrisho Kikwete is inviting us, the Diaspora group to participate among 166 individuals to the Special Parliament Session on Constitutional Review to be held between February and April, 2014.
We are writing to request all members of the Diaspora if you will be available for the session or if you know anyone who will be able to travel to Dodoma and attend the Special Parliament Session for the Constitution Review.
We are required to send 9 names to the President’s Office in Tanzania before January 2nd, 2014. For timely processing of the names (in case we will have more than 9 names). Please respond to this email with names,contact information and Bio before the end of the day December 31st, 2013.
Our presence to the Parliament’s Special Session is very crucial, as important issues like Dual Citizenship will be discussed. So, please take this message very seriously and for sure it will make a big difference if we will be present in Dodoma to argue our cases.
Let us know if you have any question
With Kind Regards,
Dr. Ndaga Mwakabuta,
DICOTA President.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako