Na Abdulaziz Video, Kilwa
Mtu mmoja
aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo
iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa
maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo
katika bandari ya Kilwa masoko.
Akiongea na Globu
ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw.
Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni
ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji
ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo
Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila
Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta
na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado
hazijajulikana
Meli hiyo ikiwa imezama majini katika gati la Kilwa Masoko
Sehemu ya chini ya meli
MERCI III kabla ya kuzama
Meli ikiwa majini
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako