A

A

Mwingereza wa asili ya Sierra Leone akamatwa JNIA akiwa na kete 95 za cocaine


Hellen Mlacky, HabariLeo — RAIA wa Uingereza Abdu Koroma (33), amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na kete 95 za dawa za kulevya aina ya kokeni zilizokuwa tumboni.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa usiku wa kuamkia jana saa 9 usiku.

Koroma ambaye ni mzaliwa wa Sierra Leone alikuwa akitoka Brazil kuja Tanzania kupitia Ethiopia ambapo aliingia na ndege ya Shirika la Ethiopia (Ethiopia Airline).

Alisema mtuhumiwa huyo alipoingia walimshtukia na baada ya kumkagua waligundua kwamba ana dawa za kulevya tumboni. Alisema pipi zote 95 alizitoa kwa njia ya haja kubwa na kwa sasa wanaendelea kumhoji. Alisema uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako