Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa Mawaziri kutoka nchi
za Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa
vijana wa nchi hizo. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika nchini Afrika
Kusini katika Mji wa Cape Townleo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya
kuufunga rasmi huku akisindikizwa na washiriki baada ya kutoa hotuba
(BEYOND THE COMMITMENT) iliyosisimua wajumbe wa mkutano huo.
Mawaziri
wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiapa
kwa niaba ya nchi zao kutekeleza majukumu waliyopitisha kwenye kikao cha
High Level Group, kuhusiana na elimu ya afya ya uzazi ( comprehensive
sexuality education and sexual and reproductive health services)
mwishoni mwa kikao cha siku mbili kilichofanyika huko Cape Town.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa
UNAIDS, Bwana Michel Sidibe wakionyesha umuhimu wa dhana nzima ya
mkutano wa High Level Group ( YOUNG PEOPLE TODAY, TIME TO ACT NOW)
kuhusiana na masuala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vjijana katika nchi
za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Julitha Onabanjo, Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA kwa hotuba aliyoitoa wakati wa kufunga mkutano
wa siku mbili wa Mawaziri wa Elimu na Afya kutoka katika Nchi za
Mashariki na Kusini mwa Afrika huko Cape Town.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano waqkisikiliza hotuba ya ufungaji iliyokuwa
ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Cape Town nchini Afrika
Kusini.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na viongozi waandamizi
waliohudhuria mkutano wa High Level Group hukom Cape Town wakisimama kwa
dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka hayati Rais Nelson Mandela. Kutoka
kushoto ni Bwana Enver Surty, Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika
Kusini, Dr. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana, Mama Salma, Bwana
Luiz Loures, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNAIDS, Dr. Julitha Onabanjo,
Naibu Mkurugenzi Mkuu, UNFPA, Bwana Qian Tang, Naibu Mkurugenzi
Mkuu-Elimu- UNESCO, Bwana Geeta Rao Gupta, Naibu Mkurugenzi Mtendaji,
UNICEF. Picha zote na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako