A

A

MH:EDWARD LOWASSA KUONGOZA TAMASHA LA BODABODA JIJINI DSM


Tamasha la Bodaboda(Boda boda Day) linatarajia kufanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders,Kinondoni. Mgeni Rasmi atakuwa Mh.Edward Lowasa,ambapo kuanzia saa moja asubuhi wale madereva wa Wilaya ya Temeke wataanzia uwanja wa Taifa,Ilala wataanzia nyuma ya TBC,Tazara,Kinondoni wataanzia katika viwanja vya biafra,maandamano yataelekea katika viwanja vya Leaders ambapo yatapokelewa na mgeni Rasmi mh.Lowasa.

Maandamano yataongozwa na askari wa uasalama barabarani na ukifika utakabidhiwa t-sheti yako.
Lengo la tamasha hilo ni kuzindua saccos ya bodaboda na chama cha waendesha bodaboda Jijini Dar,na kujiunga na mfuko wa bima ya afya.
Wasanii mbalimbali watakuwepo kwa ajili ya kutoa burudani ambao ni Linex,Amin,Barnaba,Makomandoo,Walter,Aslay na Ney wa Mitego.
Tamasha limedhaminiwa na CLOUDS FM na PSPF

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako