A

A

KINANA AANZA ZIARA CHUNYA KWA MAFANIKIO ,AVUNA KATIBU WA CHADEMA WILAYA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya unavyoendelea,kulia kwake ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya Mhandisi James Nyabakari,na Mhandisi wa kampuni ya China Communication Construction Construction kutoka China Mr.Jobs Lin ,wengine pichani ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ,Mwenyekit wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Mbozi Ndugu Godfrey Zambi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Ujenzi wa Barabara ya km 36 ukiendelea barabara hiyo inaunganisha Mbeya na wilaya ya Chunya na baada ya hapo itaunganisha mpaka mkoa wa Tabora .


Kijana Frank Robert Mwapololo ambaye anafanya shughuli za uchimbaji madini katika kundi la wachimbaji wadogo akirejesha kadi ya upinzani kwa Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu kutembelea kituo cha mafunzo cha wachimbaji wadogo cha Matundasi na kufanya mazungumzo na wachimbaji hao ambao walitoa malalamiko yao juu ya gharama za leseni,riba ya mkopo na utaratibu mzima wa kupata mkopo ni mgumu kwa hasa kwa mtu anayeishi vijijini pamoja na ukosefu wa vifaa vya kuchimbia.

Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Chunya Brayson Mwasimba akirudisha kadi yake na kujiunga rasmi na CCM baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuhutubia kwenye viwanja vya Lupa, wilaya ya Chunya.

Brayson Mwasimba akionyesha kadi yake mpya inayomuonyesha yeye ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi sasa, Brayson alikuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Chunya amekiri alipotea kujiunga Chadema na akaomba wanachunya wamsamehe mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa wilaya ya Chunya.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako