Rais wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta.
Kesi
inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda ikachelewa kuanza
baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa
jinai (ICC) Kukiri kuwa hana ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi
hiyo.
Rais
wa Kenya amekanusha mashtaka ya dhulma dhidi ya ubinadamu zinazohusiana
na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Zaidi ya watu elfu
moja waliuawawa katika mapiganao hayo na maelfu yaw engine kupoteza
makazi yao.
Katika
taarifa kwa vyombo vya habari Bi. Fatou Bensouda amesema kuwa uamuzi
huo unatokana na mashahidi wawili wakuu katika kesi hiyo kukataa kutoa
ushahidi dhidi ya Rais Kenyatta.
Mmoja
wao amesema kuwa hayuko radhi kusema anayojua kuhusu kesi hiyo ilhali
wa pili amesema kuwa alidanganya katika ushahidi wake wa awali katika
kesi hiyo.
Kujiondoa
kwa mashahidi hao imemfanya kiongozi wa mashtaka kusema kuwa kesi dhidi
ya Bwana Kenyatta haifikii kiwango cha ushahidi kinachohitajika jambo
lililomchochea kuomba kesi hyo isimamishwe kwa muda ili aweze
kusawazisha na kukusanya ushahidi zaidi.
Kesi
ya Bwana Kenyatta ilipaswa kuanza huko The Hague tarehe 5 Februari
mwaka ujao . Bwana Kenyatta alishtakiwa pamoja na naibu wake William
Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang kwa makosa ya mauji, kusababisha
watu kuhamishwa kwa nguvu katika makazi yao, kusababisha mateso kwa umma
na ubakaji kufuatia ghasia zilizotokana na matokeo ya urais katika
uchaguzi huo.
Kesi
ya Kenyatta na naibu wake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na jamii ya
kimataifa haswa baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuyaondoa mataifa ya
Afrika katika uanachama wa mahakama hiyo iliyobuniwa chini ya mkataba wa
Roma. Umoja wa Afrika umekuwa ukidai mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga
viongozi wa bara Afrika.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako