Kiungo aliyepata kutamba na uzi za Mtibwa sugar, Yanga na Azam FC Abdi Kassim 'Babi' amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Universiti Teknologi MARA FC (UITM FC) ya Malaysia.
Abdi Kassim aliyefunga goli la kwanza katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza kuchezwa katika uwanja huo dhidi ya Uganda pia alipata kuichezea timu ya DT dong ya Vetnam kabla ya kurejea nchini na kujiunga na Azam FC.
Abdi Kasasim katika ukurasa wake wa facebook ameeleza kuwa amesaini na timu hiyo ambayo ataanza kuitumikia hivi karibuni.
"A.salmaalek .kwanza nigependa kumshukuru mungu..pili nigependa muwashukuru wazazi wangu pamoja na..ndungu zangu ..tatu napenda kuwashukuru viogozi wa kmkm .ki ufupi nimesaini mkataba ..wa mwka moja .timu yangu mpya itwayo( UITM.FC ) malasia" alieleza Abdi Kassim katika ukurasa wake wa Faceboo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako