DROGBA, EBOUE MATATANI KWA KUOMBILEZA KIFO CHA MANDELA DIMBANI
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki-TFF linatarajia
kuwahoji nyota wawili wa kimataifa wa Ivory Coast wanaocheza klabu ya
Galatasaray, Didier Drogba ba Emmanuel Eboue kufuatia kuonyesha ishara
katika mechi ya kumkumbuka rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson
Mandela aliyefariki dunia Alhamisi.
Baada ya Galatasaray kushinda mabao 2-0 dhidi ya SB Elagizspor katika mchezo wa Kombe la Ligi Ijumaa, nyota
hao wawili walivua fulana zao na kubakia na vesti zilizokuwa na ujumbe
kuhusu Mandela. Mara baada ya Drogba kuvua fulana yake vesti aliyokuwa
amevaa ndani ilikuwa na maandishi yaliyosema “Thank you Madiba”
akimaanisha asante Madiba wakati vesti ya Eboue ilikuwa na maandishi
yaliyosomeka “Rest in Peace Nelson Mandela” akimaanisha pumzika kwa
amani Nelson Mandela. TFF linakataza kuonyesha fulana yoyote yenye
ujumbe unaohusiana na mambo ya siasa wakari wa mechi ya soka.
Mmh - nionavyo mimi hii sio siasa kwa kua Dunia nzima imeomboleza kwa
namna zao juu ya kifo cha Madiba, kama wataadhibiwa nadhani itakua ni
kuwaonea. Inawezekana Mandela asiwe na maana yoyote kwa chama cha mpira
wa miguu cha Uturuki lakini kwa Drogba, Eboue na Waafrika kwa ujumla
Madiba ni muhimu sana.
Maoni yako tafadhali......kama unadhani Drogba na Eboue wamefanya sahihi gonga LIKE
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako