Baadhi ya wanafamilia ndugu jamaa na
marafiki wa familia ya Isaack Mruma wakiwa wamebeba sanduku
lililohifadhi mwili wa marehemu Jerri Isaack Mruma ambaye ni Mtoto wa
Mhariri Mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN),
Isaack Mruma aliyefariki hivi karibuni jijini Nairobi Kenya kwa
kunyongwa na watu wasio julikana.
Mwili wa Jerry umewasili nchini leo
na ndege ya shirika la Kenya Airways na anataraji kuzikwa kesho mchana
makaburi ya Kinondoni baada ya ibada itakayo fanyika Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach.
Watoto wa Isaack Mruma, Kelvin Mruma
(kulia) na kakayake Khan Mruma wakipeana faraja pamoja na mwanafamilia
mwenzao wakati wa kusubiri mwili wa ndugu yao.
Baadhi ya wanafamilia.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako