Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
BAADA
ya safari ya takriban saa nne angani, hatimaye timu ya soka ya taifa ya
Bara, Kilimanjaro Stars imeatua salama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Kenya tayari kuwania taji la nne la Kombe
la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
Katika
michuano hiyo inayoanza kutimua vumbi Novemba keshokutwa, Stars
imepangwa Kundi B pamoja na Zambia, Burundi na Somalia na itafungua
dimba na Chipolopolo Alhamisi Uwanja wa Machakos.
Stars
imetua hapa saa 2:45 usiku baada ya safari ndefu kidogo wakipitia
Kigali, Rwanda kabla ya kutua Nairobi na iliwachukua saa nzima hadi
kupanda basi kuelekea hotelini baada ya kukamilisha taratibu za kuingia
nchini hapa za Idara ya Uhamiaji.
Stars
iliagwa leo mchana kwa hafla fupi kambini kwao katika hoteli ya
Accomondia jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa bendera na Katibu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya.
Katika
hafla hiyo, kocha wa Stars, Mdenmark Poulsen pamoja na kumtaja beki
Kevin Yondan kuwa Nahodha mpya, pia amesema kwamba lengo moja kubwa
kupigana kukata tiketi ya kucheza Robo Fainali kutoka kwenye Kundi lao
B, na baada ya hapo mapambano mengine yatafuatia.
Amesema anafurahi wachezaji wake wako tayari sana kwa ajili ya mashindano hayo na wamemuahidi kufanya vizuri. Nahodha mpya, Yondan kwa upande wake alisema kwamba amefurahia wadhifa huo na kwa pamoja na wachezaji wenzake, wanaahidi kwenda kupigana kurejesha heshima ya timu yao iliyopotea kwa sasa. “Tunaahidi kwenda kupigana na Mungu atatujaalia tutarudi na Kombe na kurudisha heshima yetu, kwa sababu timu yetu kwa sasa ni kama imeshuka hivi na kupoteza heshima yake mbele ya wananchi, ila tukirudi na Kombe hapa, heshima itarudi,”alisema. Mkuu wa Msafara wa Stars iliyotwaa Kombe la Challenge mara tatu, 1974, 1994 na 2010, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema wanakwenda Nairobi, Kenya kupigana kwa nguvu zote kuhakikisha Kombe la Challenge linakuja Dar es Salaam. Wachezaji walitua na Stars hapa ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam). Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam) na washambuliaji Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Mrisho Ngasa (Yanga).
Kutoka kulia Deo Munishi, Mrisho Ngassa na Bin Zubeiry
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba 1 mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
![]() |
| Wachezaji wa Kili Stars wakishuka kwenye ndege Uwanja wa Jomo Kenyatta usiku huu |

| Bin Zubeiry na Juma Luizio kushoto |
Kutoka kulia Deo Munishi, Mrisho Ngassa na Bin Zubeiry
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba 1 mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako