Ilikua ni mwezi november tarehe 26 mwaka 2012 majira ya sa 2 usiku ndipo
ziliposambaa taarifa za kifo cha muigizaji na msanii wa muziki wa
kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ Husein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’.
Leo tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya
kumkumbuku ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga.
Jana tarehe 25 november kulikua na mkesha maalum,Mkesha huu umeambatana
na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa madrasa,Miongoni mwa
watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki
mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
millardayo.com imepiga exclusive interview na mama mzazi wa Sharo
Milionea pamoja Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo
Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel,Azam
pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
‘Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua
ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka
sasa mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa
jumla ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi
rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na
mjomba wake,nikamwambia mjomba wake akiuze kwa sababu ya usumbufu maana
mi nipo mbali huku,maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa
marehemu kwa hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli Mudy
Suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia rafiki
zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa hiyo
movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa ni movie moja ambayo amecheza
yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako