Msanii wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Ndugu Haji Noorah ambaye Kimziki/Sanaa anafahamika kwa Jina la Noraah A.K.A Baba Stylez(Starz) akizungumza na Vyombo vya Habari kuhusiana na Mwenendo wa Afya Yake.Habari Kwanza Blog imekutana na Msanii Noorah kujua hali ya Afya yake"Kimsingi naendeea Vizuri kwa sasa,Nilikuwa nimelazwa Hospitali ya Kairuki(Mikocheni Mission Hospital) kwa tatizo la Tumbo,Nimekuwa nikizumbuliwa na Tumbo kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ninatatizo la Vidonda vya tumbo kumbe ndivyo Sivyo,Baada ya Vipimo vya Madaktari wamegundua ninatatizo kwenye Utumbo wangu,hivyo wameshaanza kunifanyia Matibabu na hali yangu imeendelea Kuimarika kadri ya siku zinavyo kwenda".Alisema Noorah.
Hit Maker wa Lugha Gongana Noraah anaongeza "Rai yangu kwa Watanzania na Wasanii wote tuwe na tabia ya Kufanya Uchunguzi wa Afya Zetu,Mimi nimekuwa na tatizo hili kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ni tatizo la kawaida tu,baada ya kupima nimegundulika na tatizo kwenye Utumbo wangu,nashukuru Mungu sana Madaktari wamefanya kazi kupitia Operesheni ya Tumbo,hivi sasa naendelea Vizuri".
Noorah amewashukuru sana Wasanii wote na Watanzania wanaoendelea kumuombea na kumjulia hali yake,Hii inaonesha ni nanma gani Wasanii tunatakiwa kitu kimoja wakati wa Shida na Raha.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ndugu Addo Novemba Mwasongwe akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya Kuwasili na Ujumbe wake Nyumbani kwa Msanii Noorah kwaajili ya Kumjulia hali yake na kutoa mchango wao kwaajili ya Afya ya Msanii Noorah.Addo Tanzania amesisitiza Umoja miongoni mwa Wasanii wakati wote,Shirikisho linaomba Wasanii kusaidiana katika Shida na Raha,"Tumekuaja kumuona Noorah kwasababu ni Mwanamuziki Mwenzetu na amekuwa bega kwa bega kwenye sanaa yetu,Shirikisho linatoa Rai kwa Wasanii na Watanzania kuja kumuona Msanii mwenzao hapa Nyumbani,kumjulia hali na hatimaye Uwe utamaduni wetu kwa Wasanii wote tunapopatwa na Matatizo."Alisema Addo.Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ndugu Samwel Braiton alimaarufu Braiton Mtz na Mmiliki wa Backyard Reckords akizungumza na Vyombo vya Habari nyumbani kwa Msanii Noorah hii leo alipofika kwaajili ya Kumjulia hali.Kubwa zaidi Braiton amewaomba Wasanii kujenga Utamaduni wa Kusaidiana na Kujuliana hali,haitakuwa afya sana hadi mtu apate tatizo kubwa sana ndipo watu waanze kujitokeza"Nawasanii Wasanii wote tuungane katika hali yoyote na tujenge utamaduni wa kujuliana hali". Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzinia Ndugu Addo Novemba Mwasongwe akikabidhi Mchango wa Fedha Taslimu Laki tano kwa Msanii Noorah hii leo walipofika Nyumbani kwake kwaajili ya Kumjulia hali yake ya Kiafya.Ujumbe kutoka COSOTA,Kushoto ni Philemon Kila Ofisa Msajili wa Umiliki kazi za Wasanii,katikati Msanii Noorah na Kulia ni Ofisa kutoka COSOTA anayeshughulikia Teknolojia na Mawasiliano.Hapa ni Mkurugenzi wa Habari Kwanza Media/Blog Ndugu Sanga Festo akiwa katika Picha ya pamoja na Msanii Noorah baada ya Kumtembelea Nyumbani kwake Sinza-Darajani hii leo.
Hivi Sasa Noorah anaendelea na Matibabu katika Hospital ya Mikocheni(kairuki) kwa mfumo wa Kliniki na anatarajia kuhudhuria Kliniki baada ya wiki mbili kaunzia sasa.Jumla ya Gharama zake za Matibabu hadi sasa zimefikia Milioni 2.7,Wasanii/Watanzania mnaomba kuungana na kutoa sapoti yenu kwa ndugu Yenu na Msanii wenu Noorah katika kipindi hiki cha Kurejesha afya yake katika hali ya kawaida iliaendelee na majukumu ya Kila siki katika sanaa na Maisha yake binafsi.
Picha na Habari kutoka kwa Sanga Festo wa Habari kwanza Media/blog