WANANCHI
wenye
hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.
hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.
Kijana huyo mkazi wa Mwanza
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa
12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za
kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema
“mimi nilikuwa na wenzangu sita,
wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”
wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”
“Lakini mimi kwa bahati
mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo
ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”
Hata
hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo
wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa
hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka
kwao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza
hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo
walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea
kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.
“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa
tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa
baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi
mmoja wa maeneo hayo.
Hata hivyo baadhi ya
wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi
Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo
ingawa walipewa taarifa mapema.
“Sisi tumepiga simu kituoni
hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio
limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe”
alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea
mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi
hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali,
haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.
Mtanzania lilibisha hodi
katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata
uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema
hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya
kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.
Aidha wakuu hao OC CID (ASP)
M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati
Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili
kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako