Mapokezi ya Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,nje ya viwanja vya ofisi ya Magereza wilaya ya Sumbawanga Mjini.Mh:Mwigulu Nchemba akiwasili kwenye gereza la Sumbawanga tayari kwa kukagua miundombinu na kusikiliza kero za wafungwa.Mwigulu Nchemba alipowasili kwenye Ukumbi wa halmashauri ya Sumba wanga tayari kwa kuzungumza na askari polisi wa idara zote.Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Rukwa akitoa taarifa ya mwenendo wa idara ya Uhamiaji kwa mkoa wa Rukwa na wilaya zake.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Mh.Mwigulu Nchemba akikagua makazi ya askari wa magereza Halmashauri ya mji wa sumbawanga.
Msafara wa Mwigulu Nchemba ukiendelea kujionea hali halisi ya makazi duni ya askari wa magereza wilaya ya Sumbawanga Mjini.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Mh.Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Rukwa akiwa ametokea mikoa ya Iringa,Mbeya na Songwe ambako mbali ya kukagua hali ya Magereza,pia alitembelea mipaka ya nchi yetu ukiwemo ule wa Tunduma,Vilevile ameendelea na safari yake ya kuzungumza na idara zote za jeshi la polisi ikiwa ni njia ya kuwatia moyo,kujifunza changamoto za kazi zao na kuwaelekeza dira ya wizara katika Usalama na amani ya nchi yetu.
Katika ziara yake Mkoani Rukwa,Mwigulu nchemba amepokea kero za wafungwa ikiwamo msongamano gerezani,kucheleweshwa kwa kesi na tatizo la kubambikiziwa kesi na baadhi ya askari wa jeshi la polisi.Mwigulu ameahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kushirikiana na wizara ya Katiba na sheria ili wafungwa waliokata rufaa na mahabusu wa muda mrefu majarada yao yafanyiwe kazi kwa haraka.
Akizungumza kuhusu mkakati wa wizara kuboresha makazi ya askari wake,Mwigulu anasema "tumejipanga kuhakikisha tunatumia rasilimali watu tuliyonayo ya wafungwa kuhakikisha wanatufyatulia tofali za kutosha,serikali inakwenda kukusanya sementi na vifaa vingine vya ujenzi tayari kwa safari ya makazi mapya na yakisasa.Ilimradi eneo lipo la kujenga nyumba na gereza kubwa la kisasa,tuachieni kazi sisi tukahangaike na fedha za kununulia vifaa tu,ujenzi na kufyatua tofali tutatumia wafungwa wenye sifa za kufanya kazi hiyo.
Picha/Maelezo na Festo Sanga
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako