


Katika kikao cha pamoja cha wananchi,Uongozi wa serikali na uongozi wa KPL(Kilombero Plantation Limited),Mwigulu Nchemba amepokea hatua za awali za wataalamu na watafiti wa serikali waliobobea kubaini chanzo cha mimea kuharibika kwa kiasi kikubwa hivi,Wataalam hao wamemhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa watatoa ripoti yao kamili ndani ya muda wa siku 21 ili kubaini aliyesababisha mimea ya mpunga kuungua.
Mwigulu Nchemba amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya Rais.Magufuli imejipanga kutetea haki za wananchi na itamuwajibisha yeyote anayehujumu kilimo na ustawi wa Taifa letu




Wakati wa ziara hiyo,Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya kilimo ameendelea kusisitiza kuwa kuna haja kama Taifa kuachana na kilimo cha jembe la mkono,lakini matumizi ya mbegu bora na mbolea bora ni muhimu yazingatiwe.
Wizara inajipanga kuandaa mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa kupata pembejeo kwa wakati na upatikanaji wake uwe rahisi.
Lakini,Mwigulu Nchemba pia amewasihi sana wawekezaji kwenye mashamba n.kuheshimu taratibu za uwekezaji,ili kuondoa mahusiano mabaya kati ya muwekezaji na wananchi.
Mwisho,Mh.Mwigulu Nchemba anaendelea na ziara yake ya kukagua vituo vya utafiti,Mashamba ya mbeguna,Mifugo na uvuvi katika Mkoa wa mbeya kuanzia tar.5/03/2016.
Picha/Maelezo na festo Sanga
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako