F
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.
Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.










Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais J.Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.
Picha/Maelezo na Festo Sanga
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako