A

A

YULE SENATOR BITOZ WA KENYA,HII LEO AMEBEBA HEADLINE HII HAPA

MIKE-SONKO-e1420670792211 
Senator wa Nairobi Mike Sonko huenda watu wengi wakamfahamu zaidi yeye kuliko viongozi wengine walio
kwenye ngazi za juu Kenya, mavazi yake.. maisha yake.. viko tofauti sana na jinsi viongozi wengine walivyo.
Hii ni story kubwa ambayo nimekutana nayo leo imeandikwa zaidi kwenye mitandao ya Kenya, inahusu Senator huyo kujiuzulu kutokana na kutajwa kwenye Ripoti ya kashfa ya Rushwa, ambapo jana March 31 2015 Taasisi ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi Kenya ilitaja majina zaidi ya 100 ya watu ambao wako kwenye kashfa za rushwa.
Baada ya jina lake kutajwa alikuwa kiongozi wa kwanza kutangaza kujiuzulu huku akisema kwamba anahitaji kazi ya uchunguzi juu ya kashfa hizo ifanyike kwa uhuru kabisa huku yeye akiwa nje ya ofisi yake.
Sonko amesema anatii sheria za nchi yake, anamheshimu Rais Kenyatta kwa hiyo anachokifanya ni kupisha uchunguzi kama ambavyo Rais Kenyatta ameagiza kwamba kila aliyetajwa anatakiwa aachie ofisi ili ufanyike uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Headlines zenye story za Senator huyu ni nyingi, lakini moja ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara ni ishu ya wapi anatoa pesa za kutolea huduma kama za magari ya Ambulance, Breakdown, Zimamoto, bure kabisa kwa watu wake wa Nairobi?
Story ambayo imeripotiwa na Radio Jambo Kenya iko hapa, play usikie Interview ya Sonko..

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako