Kwa ufupi
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.
Dar es Salaam. Mwanamke aliyetambulika kwa jina
la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya
Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele
akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) visiwani
Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.
Tukio hilo la aina yake lilitokea
jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na
mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio,
Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo
na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo
walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.
Hawa
akizungumza na gazeti hili alidai kwamba Ameir ni mume wake walifunga
ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja
alifariki dunia.
“ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa
kuoa wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne
na kuwaacha mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alidai Hawa.
Alidai
kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka
sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke
aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“ Naumia wanangu sijui
wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga
kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa
ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe haki yangu ili niishi
mwenyewe,” alisema Hawa.
Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai
kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke
huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye
alikiri ni mwanaye.
“ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia,
lakini sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake
mengine, mimi nilimpeleka kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini
yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.
Akizungumzia tukio hilo Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo
limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia.
“Tulivamiwa na wanawake
kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha,
mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu
walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema.
Alisema kwamba
waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na kuwachukua
wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako