Weka mbali na watoto! Prizenta asiyekaukiwa matukio wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ anadaiwa kutia aibu ukumbini baada ya kutaka kuzikunja na Master of Ceremony (MC) kisha kuumbuliwa na kigauni cha kihasarahasara alichokuwa ametupia.
Tukio hilo lililoibua gumzo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye shughuli ya ya kuzaliwa (birthday) ya shosti wake ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani kupitia Kituo cha Redio Planet FM cha mkoani hapa, Warda Makongwa.
Katika tukio hilo lililochukua nafasi kwenye Ukumbi wa White House mjini hapa, Dida alishuhudiwa akizama ukumbini humo akiwa mpole na mwenye kujificha kufuatia kuvaa kihasara lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo alivyokuwa akichangamka.
Kuna wakati mtangazaji huyo alinyanyuka na kwenda kumvaa mwimbaji nyota wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Amigo kisha akamgeuza na kumkatia mauno kabla ya kutaka kushikana na MC Chuma aliyekuwa anaongoza shughuli hiyo.
“Mh! Lakini naye Dida jamani kigauni gani kile kinaonesha hadi mambo ya ndani!” alisikika mmoja wa mashabiki wa Dida aliyekuwa ukumbini hapo.
Ili kuziba watu midomo, Dida alizama kwenye waleti yake akaibuka na ‘Misimbazi’ ambayo alimmwagia Warda na kuibua minong’ono kuwa yupo njema kimkwanja
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako