Mbaba
Kibole Kalepe akiwa darini kuepusha kipigo baada ya fumanizi. Tukio
hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka
huumaeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye
Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole
wakifanya yao.HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya
kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni
aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi
(pichani) kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo,
Ijumaa lina mkasa kamili.
Mke wa mtu, Asha Hemedi akihamaki baada ya fumanizi.
SIKU YA TUKIO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Fikiri ambaye ni dereva wa
masafa marefu aliaga kwamba anasafiri lakini akiwa hajafika mbali, gari
liliharibika na kurudi nyumbani kuchukua vifaa na kabla hajagonga
mlango, alisikia sauti ya mkewe na Kibole.
Mke wa mtu, Asha Hemedi akitaitiwa eneo la tukio. UVUMILIVU WAMSHINDA
Chanzo hicho kilizidi kushusha mistari kwamba, baada ya kusikia sauti
hizo, Fikiri hakuweza kuvumilia aliamua kuwakatisha kwa kuwagongea
mlango huku akitaja jina la mkewe ili amfungulie lakini hata hivyo
ilichukua muda mrefu mlango kufunguliwa.
Makamanda wa Polisi wakimsindikiza Kibole Kalepe kwenye gari kuelekea kituo cha Polisi Magomeni. MLANGO WAFUNGULIWA
“Mume aliendelea kugonga mlango, baada ya muda mrefu kupita ukafunguliwa ambapo mke alikutwa akiwa ameloa jasho na kuhema kwa kasi kutokana na hofu, hata hivyo alikua amefunga khanga moja tu...
Mke wa mtu Bi. Asha Hemedi naye akichukuliwa na Polisi kuelekea kituoni.MGONI JUU YA DARI
“Mume alipoangalia kila kona kumtafuta mwanaume aliyekua naye hakumuona na alipochungulia darini alimuona mgoni wake amejificha, baadaye aliomba wapigiwe simu polisi waje kumuokoa,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, wananchi wapenda mambo ya watu waliokuwa
wamezingira nyumba hiyo walimwambia yeye ni mwizi hivyo watamshushia
kipondo hevi, mgoni huyo alikataa na kudai kwamba hakuwa mwizi bali
mgoni hivyo wasimuue.
Raia wakiwazodoa wagoni wakati wakipelekwa Kituo cha Polisi Magomeni. POLISI WAMTAITI
Wananchi walimuelewa
wakaita polisi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshusha darini
kisha kumkamata na mwananke wakawapeleka Kituo cha Polisi Magomeni
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako